Hadithi katika kitabu hiki zinalenga kumwezesha mwanafunzi kutambua tamaduni nzuri na hasi, kutaja ndege mbalimbali wa porini na jinsi ya kuwatunza ndege wa nyumbani, kuelewa umuhimu wa kushiriki katika michezo mbalimbali na kula vyakula vyenye kuleta afya bora mwilini huku wakiepuka vyakula vinavyodhuru afya zao jinsi ilivyopendekezwa katika Mtaala wa Umilisi. Kwa hivyo, kitabu hiki kitafaa sana katika ufunzaji na ujifunzaji wa mada kama vile Culture (Social Studies), Ndege wa Porini (Kiswahili), Care for Domestic Animals & Living Better with Wild Animals (Agriculture), Sports (PHE) na Afya Bora (Kiswahili).
Wakulima Chipukizi na Hadithi Nyingine
Brand :
KSh300.00
Huu ni mkusanyiko wa hadithi fupi fupi zenye matukio ya kuelimisha na kusisimua. Zinajumuisha wahusika chipukizi wanaotumia ujuzi na umilisi waliojifunza darasani pamoja na vipawa vyao kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mabadiliko mazuri katika jamii.