Kitabu hiki kinalenga kunoa ubunifu miongoni mwa wanafunzi, kuwachochea kushiriki katika utunzaji wa mazingira na kuwafunza jinsi ya kuishi vyema na wanyama wa porini jinsi ilivyopendekezwa katika silabasi mpya. Kwa hivyo, kitabu hiki ni rasilimali muhimu sana katika ufunzaji na ujifunzaji wa mada kama vile Wanyama wa Porini (Kiswahili), Living Better with Wild Animals (Agriculture) na Water Pollution (Science and Technology) pamoja na kukuza mshawasha wa kuzuru maeneo mbalimbali ya nchi kama watalii
Masaibu ya Juma na Bintiheri
Brand :
KSh325.00
Mapumziko ya Agosti yanakaribia. Mwalimu Kibahaluli anawaambia wanafunzi wake kuwa wazazi wao wamewaandalia ziara ya kukata na shoka. Ziara hiyo haitakuwa ya kiburudani tu bali pia itawafaa katika kupata majibu ya chemshabongo atakayowapa. Juma, Bintiheri na wanafunzi wenzao wanasubiri likizo ya Agosti kwa hamu na ghamu. Je, Mwalimu Kibahaluli atawapa chemshabongo gani mara hii? Je, safari hiyo itawapeleka wapi?