Maswali ya Kiswahili ya K.C.S.E huwa muhimu katika kumwonyesha mwanafunzi jinsi maswali hutungwa katika mtihani. Kudurusu mada kwa kuandika husaidia pakubwa katika kumarisha uelewa wa mtu yeyote na katika kuhifadhi stadi na hatua mbalimbali. Kwa mada ambazo hutahiniwa mara kwa mara, njia za tahini hazitofautiani sana jambo ambalo hufanya dhana zinazolingana kutokea tena. Baada ya mwanafunzi kujaribu kujibu swali na kunoa, anafaa arejelee mada hiyo kama alivyofunzwa darasani au atafute ushauri wa mwalimu mpaka aweze kujibu swali au maswali kwa njia iliyosahihi. Kukata tamaa humzuia mwanafunzi kuelewa dhana mbalimbali katika Kiswahili.
Kupita katika somo la Kiswahili ni rahisi! Uwe tu makini darasani, fanya mazoezi mengi ya ziada, uwe na mtazamo chanya na ujiamini!!!!!!!!