Mashujaa wa Korona

Brand :
KSh350.00
Made Familiar

Shule zinapofungwa kwa likizo ndefu kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Korona, Kasala na wenzake wanaamua kushiriki katika mchezo wa kandanda kwenye uwanja wa kuchezea mtaani. Hata hivyo, uwanja huo unafungwa kuzuia kuenea kwa Ugonjwa wa Korona. Wanaamua kushiriki katika miradi mbalimbali. Shule zinapofunguliwa baada ya chanjo ya Korona kuvumbuliwa, kina Kasala wanapata umaarufu shuleni kutokana na mradi walioanzisha katika msimu wa likizo ndefu ya Korona. Je, ni mradi gani huu ambao umewafanya kutawazwa kama mashujaa?

Author: Alex Kinyua

Kitabu hiki kinalenga kukuza umilisi wa ubunifu, hamu ya ujifunzaji, stadi za maisha, ujuzi wa kilimo, kutumia vizuri muda wa ziada na michezo mbalimbali. Kwa hivyo, kitabu hiki ni muhimu sana katika ufunzaji na ujifunzaji wa mada kama vile Creeping Crops (Agriculture), Living better with wild animals (Agriculture), Sports (PHE) & Good use of leisure time (Home Science) jinsi ilivyopendekezwa katika Mtaala wa Umili.

Level