Kitabu hiki kinalenga kunoa ubunifu miongoni mwa wanafunzi, kuwachochea kushiriki katika utunzaji wa mazingira na kuwafunza jinsi ya kuishi vyema na wanyama wa porini jinsi ilivyopendekezwa katika silabasi mpya. Kwa hivyo, kitabu hiki ni rasilimali muhimu sana katika ufunzaji na ujifunzaji wa mada kama vile Wanyama wa Porini (Kiswahili), Living Better with Wild Animals (Agriculture) na Water Pollution (Science and Technology) pamoja na kukuza mshawasha wa kuzuru maeneo mbalimbali ya nchi kama watalii.
Ndoto za Juma na Bintiheri
Brand :
KSh300.00
Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, wanafunga safari ya Mbuga ya Wanyama ya Tsavo West na Mzima Springs pamoja na wazazi wao. Wanayoshuhudia na kujifunza katika ziara hiyo yanachochea ndoto zao kuhusu kutunza mazingira na kuishi vyema na wanyama wa porini. Pia, yanawafunulia kichemshabongo walichopewa shuleni na mwalimu Kibahaluli. Je, watapata majibu sahihi ya kichemshabongo hicho na kuibuka wanafunzi bora shuleni kwa ubunifu? Jiunge na Juma na Bintiheri katika safari hii ya kiuhalisia na kifantasia iliyojaa vitushi, patashika, mafunzo na vichekesho kwa kusoma hadithi hii ya kusisimua.