Wendi Aokoa Jahazi

Brand :
KSh350.00
Made Familiar

Wendi amepewa fursa ya kushiriki katika mchezo wa kuigiza utakaoandaliwa siku ya wazazi shuleni. Lakini anaogopa kuigiza mbele ya watu. Anajiambia kuwa hawezi kushika mistari ya wahusika. Badala yake, anaamua kupamba jukwaa la maigizo. Siku chache kabla ya maigizo kuandaliwa, mhusika mkuu anapata ajali. Bila mhusika huyu, mchezo hautaandaliwa. Je, Wendi atafanya nini ili kuwaokoa wenzake? Je, ataweza kujiamini na kupata ujasiri wa kuchukua nafasi ya mhusika mkuu na kuigiza mbele ya watu?

Author: Orpha Ramogi

Kitabu hiki kinalenga kukuza umilisi wa kujiamini, mawasiliano na ushirikiano, utunzaji wa mazingira, majanga na jinsi ya kuyazuia na uigizaji. Kwa hivyo, kitabu hiki ni muhimu sana katika ufunzaji na ujifunzaji wa mada kama vile Conserving our Environment (Agriculture & English), Mchezo wa Kuigiza (Kiswahili & English) na Majanga na Jinsi ya Kuyazuia (Kiswahili) jinsi ilivyopendekezwa katika Mtaala wa Umili.

Level