• (0)

    Dereva wa gari Jekundu

    KSh225.00

    Toma na Bella wanataka kwenda shuleni. Wanaona gari jekundu karibu na nyumbani kwao. Dereva wa gari hilo anajitolea kuwapeleka shuleni. Je, dereva ana nia gani? Je, Toma na Bella watakubali awapeleke shuleni?

  • (0)

    Tito Anatamani Kuchora

    KSh225.00

    Tito hana vidole. Hata hivyo, ana ndoto ya kufanya kazi ya kuchora na kupaka rangi kama wazazi wake. Siku moja, mwalimu anawaambia wachore wanyama wapendao. Je, Tito atawezaje kuchora bila vidole?

  • (0)

    Ali Apigania Haki Yake

    KSh250.00

    Ali, mvulana mwenye umri wa miaka kumi, anatamani kusoma hadi chuo kikuu. Hata hivyo, nyanya yake anamwagiza kumchungia mbuzi badala ya kwenda shuleni. Ali anabuni mbinu za kurejea shuleni na wakati huo huo kuendelea kumsaidia nyanya yake. Je, juhudi zake zitazaa matunda?

  • (0)

    Maria Taabani

    KSh250.00

    Maria ana mazoea ya kulala hadi Mama amwamshe. Maria pia husahau kufanya kazi zake za shule hadi Mama amkumbushe. Mama anaenda safari ya mbali. Chacha ambaye ni kakake Maria anataka kumfunza Maria adabu kwa kukosa kumtii. Je, Maria atafanya nini ili asijipate taabani?

  • (0)

    Pango la Ajabu

    KSh275.00

    Zuheri anaanguka pangoni anapocheza mwajificho na wenzake. Baba anapoingia ndani ya pango kumwokoa, anapata kisanduku. Baadaye inatangazwa redioni kuwa polisi wanatafuta kisanduku kilichopotea. Ndani yake mna vitu vya thamani. Je, wazazi wa Zuheri watakabidhi polisi kisanduku kile?

  • (0)

    Miembe ya Ajabu

    KSh275.00

    Toma ananunua miche ya miembe. Bela hapendi miembe hiyo lakini Toma anaipanda. Toma anatunza miembe yake vizuri lakini miembe haikui. Mama na Baba wanasema miembe hiyo si ya kawaida. Je, ni miembe ya aina gani?

  • (0)

    Maandazi ya Haiba

    KSh275.00

    Haiba na marafiki zake wanataka kumnunulia Baraka zawadi anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa. Baraka anaishi na nyanya yake ambaye anaugua. Hata hivyo, kina Haiba hawana pesa za kumnunulia Baraka keki na zawadi nyinginezo. Kwa kuwa likizo imeanza, wanaamua kutafuta njia ya kupata pesa. Je, watatumia mbinu gani? Je, wataweza kupata pesa za kutosha kumnunulia Baraka keki na zawadi nyinginezo?

  • (0)

    Ndoto za Juma na Bintiheri

    KSh300.00

    Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, wanafunga safari ya Mbuga ya Wanyama ya Tsavo West na Mzima Springs pamoja na wazazi wao. Wanayoshuhudia na kujifunza katika ziara hiyo yanachochea ndoto zao kuhusu kutunza mazingira na kuishi vyema na wanyama wa porini. Pia, yanawafunulia kichemshabongo walichopewa shuleni na mwalimu Kibahaluli. Je, watapata majibu sahihi ya kichemshabongo hicho na kuibuka wanafunzi bora shuleni kwa ubunifu? Jiunge na Juma na Bintiheri katika safari hii ya kiuhalisia na kifantasia iliyojaa vitushi, patashika, mafunzo na vichekesho kwa kusoma hadithi hii ya kusisimua.

  • (0)

    Kitendawili cha Taji na Hadithi Nyingine

    KSh300.00

    Taji na Zalika ni watoto wanaopenda kutunza mazingira yao na kudadisi mambo. Wanashiriki katika visa tofauti tofauti vya kusisimua vinavyowawezesha kutambua na kujifunza mengi kuhusu wanyama na mimea mbalimbali.

  • (0)

    Wakulima Chipukizi na Hadithi Nyingine

    KSh300.00

    Huu ni mkusanyiko wa hadithi fupi fupi zenye matukio ya kuelimisha na kusisimua. Zinajumuisha wahusika chipukizi wanaotumia ujuzi na umilisi waliojifunza darasani pamoja na vipawa vyao kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mabadiliko mazuri katika jamii.

  • (0)

    Sakata za Juma na Bintiheri

    KSh325.00

    Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, pamoja na rafiki yao Lulu wanapofanya utafiti kuhusu kazi waliyopewa shuleni, wanavumbua njia kadhaa za kujipatia mapato. Je, wazazi na walimu wao watakubali na kuwekeza katika uvumbuzi wao?

  • (0)

    Mashujaa wa Mazingira

    KSh325.00

    Mazingira yamejaa aina mbalimbali za taka. Baadhi ya watu wanapata ajali zinazotokana na taka hizi kama vile kukatwa na chupa. Jerry, Tinda na wenzao wanatafuta suluhisho. Je, watafanya nini?

  • (0)

    Masaibu ya Juma na Bintiheri

    KSh325.00

    Mapumziko ya Agosti yanakaribia. Mwalimu Kibahaluli anawaambia wanafunzi wake kuwa wazazi wao wamewaandalia ziara ya kukata na shoka. Ziara hiyo haitakuwa ya kiburudani tu bali pia itawafaa katika kupata majibu ya chemshabongo atakayowapa. Juma, Bintiheri na wanafunzi wenzao wanasubiri likizo ya Agosti kwa hamu na ghamu. Je, Mwalimu Kibahaluli atawapa chemshabongo gani mara hii? Je, safari hiyo itawapeleka wapi?

  • (0)

    Wendi Aokoa Jahazi

    KSh350.00

    Wendi amepewa fursa ya kushiriki katika mchezo wa kuigiza utakaoandaliwa siku ya wazazi shuleni. Lakini anaogopa kuigiza mbele ya watu. Anajiambia kuwa hawezi kushika mistari ya wahusika. Badala yake, anaamua kupamba jukwaa la maigizo. Siku chache kabla ya maigizo kuandaliwa, mhusika mkuu anapata ajali. Bila mhusika huyu, mchezo hautaandaliwa. Je, Wendi atafanya nini ili kuwaokoa wenzake? Je, ataweza kujiamini na kupata ujasiri wa kuchukua nafasi ya mhusika mkuu na kuigiza mbele ya watu?

  • (0)

    Mashujaa wa Korona

    KSh350.00

    Shule zinapofungwa kwa likizo ndefu kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Korona, Kasala na wenzake wanaamua kushiriki katika mchezo wa kandanda kwenye uwanja wa kuchezea mtaani. Hata hivyo, uwanja huo unafungwa kuzuia kuenea kwa Ugonjwa wa Korona. Wanaamua kushiriki katika miradi mbalimbali. Shule zinapofunguliwa baada ya chanjo ya Korona kuvumbuliwa, kina Kasala wanapata umaarufu shuleni kutokana na mradi walioanzisha katika msimu wa likizo ndefu ya Korona. Je, ni mradi gani huu ambao umewafanya kutawazwa kama mashujaa?