-
(0)By : Jackson Omondi
Tito Anatamani Kuchora
KSh225.00Tito hana vidole. Hata hivyo, ana ndoto ya kufanya kazi ya kuchora na kupaka rangi kama wazazi wake. Siku moja, mwalimu anawaambia wachore wanyama wapendao. Je, Tito atawezaje kuchora bila vidole?
-
-
(0)By : Orpha Ramogi
Wakulima Chipukizi na Hadithi Nyingine
KSh300.00Huu ni mkusanyiko wa hadithi fupi fupi zenye matukio ya kuelimisha na kusisimua. Zinajumuisha wahusika chipukizi wanaotumia ujuzi na umilisi waliojifunza darasani pamoja na vipawa vyao kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mabadiliko mazuri katika jamii.
-
(0)By : Orpha Ramogi
Wendi Aokoa Jahazi
KSh350.00Wendi amepewa fursa ya kushiriki katika mchezo wa kuigiza utakaoandaliwa siku ya wazazi shuleni. Lakini anaogopa kuigiza mbele ya watu. Anajiambia kuwa hawezi kushika mistari ya wahusika. Badala yake, anaamua kupamba jukwaa la maigizo. Siku chache kabla ya maigizo kuandaliwa, mhusika mkuu anapata ajali. Bila mhusika huyu, mchezo hautaandaliwa. Je, Wendi atafanya nini ili kuwaokoa wenzake? Je, ataweza kujiamini na kupata ujasiri wa kuchukua nafasi ya mhusika mkuu na kuigiza mbele ya watu?