-
-
-
-
(0)
K.C.S.E Made Familiar – KISWAHILI
Kitabu hiki cha Mazoezi ya Insha na Lugha cha Kenya Certificate of Secondary Education
(K.C.S.E.) kimeandaliwa ili kuwafahamisha wanafunzi na maswali ya Kiswahili ya K.C.S.E. karatasi ya 1 a 2. Kitabu hiki kina maswali ya insha na lugha ya K.C.S.E. yaliyotahiniwa kutoka mwaka wa 2000 maka mwaka huu.
Masomo ya Kiswahili yamegawanywa katika karatasi tatu ambazo zimepewa nambari za kuzitambulisha kama:
- 102/1 (Insha) – Hutahiniwa juu ya alama 40
- 102/2. (Lugha) – Hutahiniwa juu ya alama 80
- 102/3. (Fasihi ya Kiswahili) – Hutahiniwa juu ya alama 80
Tanbihi: Awali, kabla ya mwaka wa 2001 somo la Kiswahili lilikuwa limegawanywa katika karatasi tatu ambazo zilikuwa 102/1A (Insha), 102/1B (Lugha) a 102/2 (Fasihi); jambo hili litadhihirika katika karatasi za mitihani ya mwaka wa 2000.
Maswali yote katika kitabu hiki yako katika hali yao asili (halisi) yaani kama yalivyotokea katika karatasi ya mtihani wa K.C.S.E. Chini au kando ya kila swali, mambo yafuatayo yameonyeshwa waziwazi:
- Alama zilizokuwa zikituzwa katika kila swali
- Mwaka wa tahini.
Mpangilio huu utawasaidia wanafunzi kutambua mada ambazo hutahiniwa mara kwa mara na njia mbalimbali ambazo kwazo dhana katika hizo mada hutahiniwa. Majibu ya maswali yametolewa nyuma ya kitabu hiki na yameandikwa kwa ukamilifu kama yanavyopaswa kuandikwa ili yaridhishe matakwa ya mtihani wa K.C.S.E.
Maelezo na maelekezo yametolewa baada ya baadhi ya majibu ili kumwonyesha mtahiniwa jinsi ya kufikia majibu yanayokubalika.