-
(0)By : Ali Attas
Sakata za Juma na Bintiheri
KSh325.00Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, pamoja na rafiki yao Lulu wanapofanya utafiti kuhusu kazi waliyopewa shuleni, wanavumbua njia kadhaa za kujipatia mapato. Je, wazazi na walimu wao watakubali na kuwekeza katika uvumbuzi wao?
-
(0)By : Orpha Ramogi
Wakulima Chipukizi na Hadithi Nyingine
KSh300.00Huu ni mkusanyiko wa hadithi fupi fupi zenye matukio ya kuelimisha na kusisimua. Zinajumuisha wahusika chipukizi wanaotumia ujuzi na umilisi waliojifunza darasani pamoja na vipawa vyao kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mabadiliko mazuri katika jamii.
-
(0)By : Joe Mirungu
Kitendawili cha Taji na Hadithi Nyingine
KSh300.00Taji na Zalika ni watoto wanaopenda kutunza mazingira yao na kudadisi mambo. Wanashiriki katika visa tofauti tofauti vya kusisimua vinavyowawezesha kutambua na kujifunza mengi kuhusu wanyama na mimea mbalimbali.
-
(0)By : Ali Attas
Ndoto za Juma na Bintiheri
KSh300.00Juma na Bintiheri, ambao ni binamu, wanafunga safari ya Mbuga ya Wanyama ya Tsavo West na Mzima Springs pamoja na wazazi wao. Wanayoshuhudia na kujifunza katika ziara hiyo yanachochea ndoto zao kuhusu kutunza mazingira na kuishi vyema na wanyama wa porini. Pia, yanawafunulia kichemshabongo walichopewa shuleni na mwalimu Kibahaluli. Je, watapata majibu sahihi ya kichemshabongo hicho na kuibuka wanafunzi bora shuleni kwa ubunifu? Jiunge na Juma na Bintiheri katika safari hii ya kiuhalisia na kifantasia iliyojaa vitushi, patashika, mafunzo na vichekesho kwa kusoma hadithi hii ya kusisimua.
-
(0)By : Elijah Sabakaki
The Broken Promise and Other Stories
KSh300.00Kibe always find himself between a rock and a hard place. To find his way out, he must apply skills from the subject he fears most—Art and Craft. Kamaria, who loves Art and Craft, often comes to his rescue. For how long will Kibe rely on Kamaria for help?
-
(0)By : Hillary Ihaji
Balozi in Trouble Again
KSh300.00Balozi always want to impress his friends. This puts him in trouble every time. He uses his creativity and imagination skills to get out of trouble and to prove himself to his peers. Read these three captivating short stories to find out how he tackles the different challenges he encounters.
-
(0)By : Hillary Ihaji
My Secret and Other Stories
KSh300.00Have you ever imagined living in a place where you are not allowed to eat, sleep, play, make friends or go to school? How does it feel to live in such a place? In this collection of short interesting stories, you will interact with children living in such a world and how they feel and cope.
-
(0)By : Ali Attas
Masaibu ya Juma na Bintiheri
KSh325.00Mapumziko ya Agosti yanakaribia. Mwalimu Kibahaluli anawaambia wanafunzi wake kuwa wazazi wao wamewaandalia ziara ya kukata na shoka. Ziara hiyo haitakuwa ya kiburudani tu bali pia itawafaa katika kupata majibu ya chemshabongo atakayowapa. Juma, Bintiheri na wanafunzi wenzao wanasubiri likizo ya Agosti kwa hamu na ghamu. Je, Mwalimu Kibahaluli atawapa chemshabongo gani mara hii? Je, safari hiyo itawapeleka wapi?
-
(0)By : Nicholas Ogal
Mashujaa wa Mazingira
KSh325.00Mazingira yamejaa aina mbalimbali za taka. Baadhi ya watu wanapata ajali zinazotokana na taka hizi kama vile kukatwa na chupa. Jerry, Tinda na wenzao wanatafuta suluhisho. Je, watafanya nini?
-
(0)By : Emmanuel Munasi
Maandazi ya Haiba
KSh275.00Haiba na marafiki zake wanataka kumnunulia Baraka zawadi anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa. Baraka anaishi na nyanya yake ambaye anaugua. Hata hivyo, kina Haiba hawana pesa za kumnunulia Baraka keki na zawadi nyinginezo. Kwa kuwa likizo imeanza, wanaamua kutafuta njia ya kupata pesa. Je, watatumia mbinu gani? Je, wataweza kupata pesa za kutosha kumnunulia Baraka keki na zawadi nyinginezo?
-
(0)By : Zawadi Namukhula
Miembe ya Ajabu
KSh275.00Toma ananunua miche ya miembe. Bela hapendi miembe hiyo lakini Toma anaipanda. Toma anatunza miembe yake vizuri lakini miembe haikui. Mama na Baba wanasema miembe hiyo si ya kawaida. Je, ni miembe ya aina gani?
-
(0)By : Jackson Omondi
Pango la Ajabu
KSh275.00Zuheri anaanguka pangoni anapocheza mwajificho na wenzake. Baba anapoingia ndani ya pango kumwokoa, anapata kisanduku. Baadaye inatangazwa redioni kuwa polisi wanatafuta kisanduku kilichopotea. Ndani yake mna vitu vya thamani. Je, wazazi wa Zuheri watakabidhi polisi kisanduku kile?
-
(0)By : Victor Olum
Siku yenye Vituko
KSh250.00Taji na Furaha wana furaha. Familia yao inaenda safarini pamoja. Je, watashuhudia mambo gani njiani? Jiunge na familia ya kina Taji na Furaha katika safari yao fupi ya kupendeza.
-
(0)By : Daniel Mwangi
Maria Taabani
KSh250.00Maria ana mazoea ya kulala hadi Mama amwamshe. Maria pia husahau kufanya kazi zake za shule hadi Mama amkumbushe. Mama anaenda safari ya mbali. Chacha ambaye ni kakake Maria anataka kumfunza Maria adabu kwa kukosa kumtii. Je, Maria atafanya nini ili asijipate taabani?
-
(0)By : Daniel Mwangi
Ali Apigania Haki Yake
KSh250.00Ali, mvulana mwenye umri wa miaka kumi, anatamani kusoma hadi chuo kikuu. Hata hivyo, nyanya yake anamwagiza kumchungia mbuzi badala ya kwenda shuleni. Ali anabuni mbinu za kurejea shuleni na wakati huo huo kuendelea kumsaidia nyanya yake. Je, juhudi zake zitazaa matunda?
-
(0)By : Jackson Omondi
Mbingu ina Rangi Gani?
KSh225.00Zawadi na Bahati wanapenda kutazama anga. Wanashangaa jinsi rangi ya angani inavyobadilika. Mara ni nyeusi. Mara ina upinde wenye rangi nyingi. Je, mbingu ina rangi gani?